Je, dirisha la usajili Ligi Kuu ya Uingereza linafunguliwa na kufungwa lini?
- Soma na hii - Dirisha la Usajili nchini Italia lafanyiwa mabadiliko
Hapa tumekuwekea mambo yeote unayotakiwa kuyajua kuhusiana na dirisha la usajili kwenye majira ya joto, ikiwa ni pamoja na lini dirisha litafunguliwa na ni lini litafungwa, maana yake kwa Ligi Kuu ya Uingereza na namna inavyokuwa kwa ligi nyingezo barani la Ulaya.
- Soma na hii - Ronaldo anataka Mreno huyu atue Real Madrid
Sababu ya mabadiliko hayo ni kuviwesha vilabu kuepuka usumbufu katika vikosi vyao mara baada ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza kuanza tarehe 11 Agosti.
Kwa maana hiyo, vilabu vinaruhusiwa kuanza kusajili wachezaji tarehe 17 Mei.
Makubaliano ya dili za uhamisho wa wachezaji yanaweza kufikiwa kabla ya Mei 17, hata hivyo, kazi ya kutia saini haiwezi kufanyika hadi dirisha litakapokuwa limefunguliwa rasmi.
Hiyo inamaana uhamisho wa ndani ya ligi unaweza kukamilika kuanzia tarehe 17 Mei usiku wa manane, lakini uhamisho wa wachezaji kutoka nje ya ligi utakamilika wakati mfumo wa uhamisho wa FIFA, "Transfer Matching System (TMS)" utakapofunguliwa rasmi tarehe 8 Juni.
Klabu zinaweza kusajili wachezaji kutoka nchi yoyote ile ili mradi tu dirisha lao la usajili limefunguliwa, ikiwa na maana kwamba vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza bado vina uwezo wa kuendelea kuuza wachezaji wake baada ya dirisha lao la usajili kufungwa tarehe 9 Agosti.
Hiyo ni kwa sababu ligi nyingine zinatofautiana na ratiba EPL na bado madirisha yao ya usajili yatakuwa wazi kwa wakati huo.
Nchini Ufaransa, dirisha la usajili litafunguliwa tarehe 9 Juni. Italia na Ujerumani litafunguliwa Julai 1 na Uhispania itakuwa tarehe 2 Julai.
Madirisha ya usajili wa ligi zote nne yatafungwa tarehe 31 ya mwezi Agosti.
Je, dirisha la usajili Ligi Kuu ya Uingereza linafunguliwa na kufungwa lini?
Reviewed by Zero Degree
on
5/16/2018 12:20:00 PM
Rating: