Loading...

Jose Mourinho aweka wazi mipango yake kwenye usajili wa majira ya joto


Manchester United wanatarajiwa kuwa 'bize' na kusaka wachezaji wapya kwenye majira ya joto.
Chini ya uongozi wa Jose Mourinho, Manchester United wameendelea kusonga mbele ukilinganisha na misimu kadhaa iliyopita. Wakiwa na pointi 71 kwa sasa, huku zikiwa zimesalia mechi 5 kabla ligi haijaisha tayari wameshavuka pointi 69 za msimu uliopita kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Lakini aibu waliyoipata kwa kutolewa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya 16 bora dhidi ya Sevilla na tofauti kubwa ya pointi iliyopo kati yao na vinara wa Ligi Kuu, Manchester City inaonyesha kuwa United bado wanahitaji kuboresha kikosi chao. Inaamini kwamba, klabu hiyo itatumia fedha ya kutosha kuongeza nguvu mpya kwenye dirisha la usajili wa majira ya joto.
Lakini Jose Mourinho amekanusha uvumi kwamba watatumia fedha nyingi na atawajibika kwenye soko la usajili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Mourinho alisema: “Hatutakuwa na matumizi makubwa zaidi ya uwezo wetu. Hatutafanya maamuzi yoyote ya kijinga.”

“Tunajaribu kufanya maboresho kidogo. Hicho ndicho tutajaribu kufanya.
“Kila mtu atajaribu kuboresha kikosi chake – kama tulivyofanya msimu uliopita, ambapo tulimaliza katika nafasi ya sita na msimu natumai tutamaliza katika nafasi ya pili.

“Msimu ujao, tutajaribu kuboresha zaidi lakini ngoja kwanza tuone kitakachotokea. Labda Manchester City watawekeza zaidi na kutoruhusu yeyote kuwakaribia, sijui itakuwaje.

“Lakini haituhusu sisi na wao, inatuhusu sisi na wao pamoja na Liverpool, Arsenal, Chelsea na Spurs. Sio Manchester City na United bali timu zote sita zitahusika.”
Jose Mourinho aweka wazi mipango yake kwenye usajili wa majira ya joto Jose Mourinho aweka wazi mipango yake kwenye usajili wa majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 4/16/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.