Loading...

Wachezaji 5 ambao wanaweza kuondoka Manchester United kwenye majira ya joto

Mourinho na Paul Pogba
Jose Mourinho amefanyiwa ukaguzi na kukoselewa mara kadhaa na mashabiki wa Manchester United tangu awasili Old Trafford kwenye majira ya joto 2016.

Kwa mujibu wa tovuti moja ya Uingereza, hapa chini ni majina ya wachezaji ambao wanaweza kuondoka Old Trafford kama Jose Mourinho ataendelea kuwa meneja.
  • Paul Pogba

Kiungo huyo raia wa Ufaransa ametimiza miaka 25 hivi karibuni. Kwa sasa ameingia katika umri wa ukomavu kwenye maisha yake ya soka, hivyo ndivyo unavyoweza kusema,  lakini bado hajafanikiwa kupata nafasi ya kuwa mchezaji tegemezi wa klabu ya Manchester United na ameripotiwa kuwa na mgogoro na meneja wa sasa Jose Mourinho. Kama Pogba atalazimisha kuondoka au la haijajulikana, muda ukifika ndio itajulikana.
  • Anthony Martial

Licha ya kuanza vizuri mwanzoni mwa msimu, Martial amepotea uwanjani tangu Dicemba. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa kama kivuli chake binafsi. Mfaransa huyo anaweza kushawishika kuondoka kama Mourinho atabaki.
  • Luke Shaw

Shaw alipata nafasi ya kuanza na kikosi cha kwanza cha United ndani ya wiki nne, lakini alitolewa nje wakati wa mapumziko baada ya kuonyesha kiwango ambacho kilionyesha wazi kuwa sababu ya Mourinho kumpa adhabu ya kukaa benchi. Hiyo inajitosheleza kuonyesha uhusiano uliopo kati ya Shaw na Jose, ambao unaweza kuchangia kuwa msukumo kwa yeye kuondoka Old traford.
  • David De Gea

Bila shaka yeye ndio mchezaji bora katika kikosi cha United kwa sasa na kuondoka kwake inaweza kuwa pigo kubwa kwao. Raia huyo wa Uhispania kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Real Madrid anaingia mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake na hajaonyesha dalili zozote za kuwa na mpango wa kusaini mkataba mwingine.
  • Marouane Fellaini

Raia huyo wa Ubelgiji anaonekana yuko njiani kuondoka Manchester United baada ya kutoka kwa ripoti iliyodai kuwa mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo juu ya mkataba mpya yamegonga mwamba. Mkataba wa sasa wa Mbelgiji huyo unaisha mwishoni mwa msimu huu na licha ya viongozi wa klabu kuendelea kujaribu kumshawishi Fellaini abaki, hakuna mabadiliko yoyote kwenye mazungumzo yao juu ya mkataba mpya.
Wachezaji 5 ambao wanaweza kuondoka Manchester United kwenye majira ya joto Wachezaji 5 ambao wanaweza kuondoka Manchester United kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 3/19/2018 09:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.