Loading...

Ronaldo anataka Mreno huyu atue Real Madrid


Baada ya kufanya vibaya kwenye La Liga msimu huu, Real Madrid itakuwa makini wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa kwenye majira ya joto kwa lengo la kuimarisha kikosi cha kwa ajili ya msimu ujao. Wachezaji wachache pia wanategemewa kuondoka ili kutoa nafasi kwa wacheaji wapya wanaotarajiwa kuingia.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anataka kusajili mchezaji mwenye uwezo mkubwa na amekuwa akihusishwa na wachezaji kama Harry Kane, Robert Lewandowski nad Mohamed Salah kuelekea dirisha la usajili kwenye majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa ya Don Balon, Cristiano Ronaldo anamshawishi Pérez amsajili Goncalo Guedes kutoka Valencia kwenye majira ya joto. Haamini kuwa klabu hiyo ina uhitaji wa kusajili mshambuliaji mwingine. Badala yake anataka Mreno mwenzake atue Bernabeu kuongeza nguvu kwenye safu ya mbele msimu ujao.

Guedes anaichezea klabu ya Valencia kwa mkopo akitokea PSG
Guedes alijiunga na Valencia kwa mkopo akitokea Paris Saint-Germain mwezi Septemba mwaka jana. Ameonyesha uwezo mkubwa katika klabu hiyo na tayari ni kipenzi cha mashabiki wengi.

Inasemekana kuwa Valencia wanataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu na PSG pia wako tayari kumuuza ili kutimiza vigezo vya UEFA. Vigogo hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa wanataka zaidi ya pauni milioni 40.

Lakini kwa kitendo cha Ronaldo kukazania uhamisho wa Mreno mwenzake, Real Madrid wanaweza kumsajili kwenye majira ya joto.
Ronaldo anataka Mreno huyu atue Real Madrid Ronaldo anataka Mreno huyu atue Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 4/15/2018 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.