Loading...

Chaguo la kwanza la Manchester City kwenye usajili wa majira ya joto

Julian Weigl
Manchester City imekuwa na msimu wenye mafanikio msimu huu katika Ligi Kuu ya Uingereza. Pep Guardiola ameonyesha mabadiliko makubwa Man City, akivunja rekodi nyingi za EPL.

Klabu hiyo inapanga kufanya matumizi makubwa kusajili wa wachezaji wapya kwenye majira ya joto licha ya kuaibika kwa kutolewa na Liverpool kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, huku wakielekeza nguvu yao kubwa kwa kiungo wa Borussia Dortmund, Julian Weigl.

Pep atampa kipaumbele kiungo mkabaji kwenye usajili wa majira ya joto kwani anatambua kuwa timu yake inamtegemea Fernandinho pekee. Awali Man City walihusishwa na kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred lakini inaonyesha Mbrazil huyo hawezi kuimudu nafasi hiyo. Zaidi ya hapo, aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona anataka mchezaji mwenye uwezo wa kupenya ni sio wa kuharibu nafasi.


Kulingana na ripoti mbalimbali, inaonekana Manchester City wataelekeza nguvu zao kwa kiungo wa Borussia Dortmund, Julian Weigl.

Mjerumani huyo anakadiriwa kuwa na thamani ya karibu pauni milioni 27 lakini Dortmund haitakuwa tayari kumuuza nyota wao kirahisi hivyo, Manchester City italazimika kulipa kiasi kikubwa cha fedha kuwashawishi wafanye biashara.

Ingawa kiungo huyo ana mkataba unaoisha mwaka 2021 lakini Dortmund hawana msukumo wowote wa kumuuza.
Chaguo la kwanza la Manchester City kwenye usajili wa majira ya joto Chaguo la kwanza la Manchester City kwenye usajili wa majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 4/13/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.