Loading...

Mtihani mwingine kwa Kocha Jose Mourinho.

NAHODHA Wayne Rooney, mkongwe Zlatan Ibrahimovic, kinda Anthony Martial na ‘assist king’ Henrikh Mkhitaryan, wamewapa mashabiki wa United walichokikosa kwa miezi mitatu sasa.

Safu kali ya ushambuliaji, yenye uchu na kasi, ambayo ni wazi kama Jose Mourinho angeanza nayo tangu Agosti, Manchester United wangekuwa kwenye nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Premier League.

Kwanini? Walipopangwa pamoja, dhidi ya West Ham kwenye robo fainali ya kombe la EFL, wakali hawa waliiongoza United kupata ushindi mnono wa mabao 4-1.

Martial na Ibrahimovic walifunga mara mbili kila mmoja, huku Mkhitaryan akibeba vichwa vya habari kwa asisti mbili alizozitoa baada ya kuinyanyasa sana ngome ya United.

Yale maneno yaliyokuwa yakisemwa kuhusu Wayne Rooney, ambayo bila shaka yataendelea kusikika, yalionekana hayana maana baada ya nahodha huyo kucheza soka la kasi na akili kubwa.

Kwa sasa, Martial na Mkhitaryan, mmoja akiwa na miaka 20 na mwingine akiwa na 27, ni wachezaji ambao Mourinho analazimika kuwatumia kuijenga safu kali ya ushambuliaji msimu huu.

Martial, ni kweli awali aliaminika sana, japo hakuwa na mwanzo mzuri. Alifunga bao moja kwenye mechi 5 alizoanza na tatu alizoingia kutokea benchi, hakuwa na mchango mkubwa kwa timu na kasi yake ilianza kupotea.

Mashabiki wa United wakabaki na maswali juu ya nini kimemkuta kinda huyu aliyesajiliwa kwa pauni mil 50 na kung’aa msimu uliopita.

Lakini bado kipaji chake kikahitaji uvumilivu, bado ni kijana anayehitaji muda wa kujifunza na kuaminika. Na hapa ndipo inapokuja sifa ya kocha mzuri katika kudili na tatizo kama hili la Martial.

Kelele zikawa nyingi nje ya uwanja kuwa Mourinho amepoteza imani na Martial, ikatajwa kuwa yuko kwenye orodha ya wachezaji watakaotemwa mwishoni mwa msimu, lakini kiwango chake dhidi ya West Ham ni majibu ya maswali yote haya.

Kwa upande wa Mkhitaryan, ulimwengu wa soka ukafahamu kwanini Mourinho aliweka mzigo wa maana kwa Dortmund ili aweze kumsajili.

Henrink ametua Old Trafford akiwa mchezaji bora wa msimu kwenye Bundesliga, ni yeye aliyekuwa muundaji wa hatari zote za Dortmund.

Alifunga jumla ya mabao 23 na kutengeneza 15, mwanzo mbaya katika kikosi cha United, mechi nane bila bao wala asisti zikaleta hofu kwa mashabiki na wapenda soka duniani.

Mkhitaryan ameanza mchezo mmoja tu wa Ligi msimu huu na mwenyewe akicheza kwa dakika 45 dhidi ya mahasimu wao, Manchester City.

Baada ya hapo, ikapita takribani miezi miwili akiwa benchi, kwanini Mourinho alimuweka benchi? Hakuna aliyekuwa na majibu.

Ikadaiwa kuwa, ni kawaida kwa Mourinho kumfanya mchezaji mmoja mfano kwa wengine pindi anapoboronga, hivyo Mkhitaryan akatolewa kafara.

Bastian Schweinsteiger, naye akashushwa kikosi cha vijana huku Luke Shaw akifokewa hadharani. Mourinho akasimama katika kile anachokiamini na hatimaye Mkhitaryan, akarudi tena uwanjani na mashabiki wa United wakampokea kwa furaha.

Schweinsteiger naye akarejea uwanjani kwenye pambano dhidi ya West Ham na hii ikatafsiriwa na wengi kama mwisho wa matatizo ya wachezaji na Jose Mourinho, United ikapata matokeo!

Kazi kubwa inayomkabili Mourinho hivi sasa ni kuhakikisha namna anavyoweza kuwalinda Martial na Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza.

Kasi yao, ubunifu wao na uwezo wa kuipenya ngome ya timu pinzani inaweza kuwa silaha kubwa katika mabadiliko ambayo Mourinho amepanga kuyapata msimu huu.

Mchezo wa kesho mashabiki wa United wanatamani kujua ni kikosi gani Mourinho atakachoshuka nacho uwanjani, kilekile kilichoimaliza West Ham au ataendelea na utaratibu wake wa kutokuwa na kikosi cha kwanza kilichocheza mfululizo?

ZeroDegree.
Mtihani mwingine kwa Kocha Jose Mourinho. Mtihani mwingine kwa Kocha Jose Mourinho. Reviewed by Zero Degree on 12/03/2016 01:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.