Loading...

Tuache kutumia dawa za antibiotiki kiholela - Waziri Ummy

Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu ameitaka jamii kuacha matumizi ya dawa za kutibu maambuzi ya Bakteria (antibiotics) kiholela jambo ambalo linapeleka usugu wa vimelea vya magonjwa.
Waziri ummy ameyasema hayo leo katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa jamii kuhusu kuimarisha huduma za afya ngazi ya msingi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF), Odo Ummy Foundation pamoja na Taasisi ya Apotheker ili kuwajengea uelewa wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii hususani ni katika sekta ya afya.

"Sasa hivi kuna matumizi yasiyo sahihi ya dawa za antibiotiki; mtoto ameumwa tumbo kidogo la kuharisha mzazi unaenda duka la dawa unanunua dawa za antibiotiki matokeo yake tumesababisha usugu wa vimelea vya magonjwa hali inayo pelekea kila dawa za antibiotiki kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Mtoto akiharisha apewe ORS - Zink. Antiobiotiki ni hadi aandikiwe na Daktari"- amesema Waziri Ummy.

"Kwa sasa matumizi ya dawa za antibiotiki yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 65% na Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kwa wagonjwa wanaolazwa tusifike asilimia 30% sasa tupo asilimia 65%"

"Mara nyingi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) hawaishi, tuna zile dhana za kusema mtoto sio ridhiki, lakini tuna msingizia mwenyezi Mungu na tumefanya vizuri kama serikali kupunguza vifo vya kinamama wajawazito kutoka vifo 556 mpaka vifo 104 katika kila wanawake 100,000, Rais Samia ameandika historia duniani na hata barani Afrika" amesema Waziri Ummy na kuongeza kuwa;

"Nimepokea ombi lako ndugu yangu Doris Mollel la kuongeza siku za likizo kutoka siku saba hadi siku 14 kwaajili ya kinababa hivyo kuwasaidia wake zao lakini kumekuwa na changamoto wengi wao hawatumii hizi siku kwaajili ya kusaidia wake zao badala yake wanatumia kufanya shughuli nyengine na baadhi hushinda baa hivyo maana ya likizo haionekani" amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera wa Apotheker, Dk. Suleiman Kimatta amesema kuwa magonjwa mengi kama vile Ukimwi,kifua kikuu,malaria kuna vimelea vinavyo sababisha magonjwa hayo hivyo ni muhimu kumeza dawa sahihi ili kuweza kuua vimelea kwani ukitumia dawa kiholela inapelekea kimelea kuwa sugu na kuhatarisha afya yako pamoja na kifo.
Tuache kutumia dawa za antibiotiki kiholela - Waziri Ummy Tuache kutumia dawa za antibiotiki kiholela - Waziri Ummy Reviewed by Zero Degree on 5/22/2024 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.