Dirisha la usajili sasa kufungwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya
Mameneja walikuwa wamelalamika kwamba nafasi ya wachezaji kuhama ligi ikiendelea hutatiza klabu na maandalizi.
Kuanzia msimu ujao, dirisha la kuhama wachezaji litafungwa saa 17:00 BST Alhamisi itakayokuwepo kabla ya ligi mpya kuanza.
Kura hiyo haikuwa kwa kauli moja na klabu bado zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi mwisho wa dirisha la kawaida la kuhama wachezaji.
Dirisha la kuhama wachezaji kote Ulaya huendelea kuwa wazi hadi tarehe 31 Agosti.
Hatua ya klabu hiyo za Ligi ya Premia ina maana kwamba ingawa klabu zitaweza kuendelea kuuza wachezaji hadi siku hiyo, ununuzi utafikia kikomo tarehe 9 Agosti msimu wa 2018-19.

Klabu za ligi nyingine za Ulaya bado zitaweza kununua na kuuza wachezaji hadi 31 Agosti.
Uhamisho wa wachezaji katika ligi nyingine ndogo za England na Wales ((Championship, League One na League Two) hautaathiriwa.
Wasimamizi wa ligi hizo wamedokeza kwamba huenda wakafuata njia hiyo ya Ligi ya Premia lakini wanahitaji mashauriano zaidi.
Klabu za Ligi ya Premia zilizounga mkono mabadiliko hayo bado hazijabainika kabisa, ingawa inaaminikakwamba zilikuwa 14 kati ya 20.

Mabadiliko hayo hata hivyo hayatafupisha muda wa klabu kununua wachezaji kwani soko litafunguliwa mapema na litakuwa wazi muda wa wiki 12, kuambatana na sheria za Fifa.
Agosti, mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane alisema kufungwa kwa soko mapema kutawezesha wachezaji kuangazia klabu zao.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Ijumaa alisema wachezaji wanahitaji "uwazi" kuhusu hali yao.
Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson pia alisema soko linafaa kufungwa mapema alipoulizwa kuhusu juhudi za Barcelona kumtaka nyota wa Liverpool Philippe Coutinho.

Msimu wa 2018-19 utaanza baada ya Kombe la Dunia ambalo litafikia kikomo tarehe 15 Julai nchini Urusi.
Dirisha la usajili sasa kufungwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya
Reviewed by Zero Degree
on
9/07/2017 07:15:00 PM
Rating: