Waziri Simbachawene, Edwin Ngonyani wajiuzulu kufuatia kutajwa kwenye sakata la madini
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene |
Uamuzi a viongozi hao umekuja baada ya Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya usalama.
Kwa upande wake, akiongea leo Alhamisi mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.
Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani |
“Hata sasa unanichelewesha nipo naandika barua ya kujiuzulu, hii ni nafasi niliyopewa na ni lazima nimuunge mkono Rais katika hatua zake za kutaka kubadili mfumo wa nchi na kuufanya wenye manufaa kwa wananchi,” amesema Ngonyani.
Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.
Waziri Simbachawene, Edwin Ngonyani wajiuzulu kufuatia kutajwa kwenye sakata la madini
Reviewed by Zero Degree
on
9/07/2017 07:43:00 PM
Rating: