Loading...

Wachezaji watano wanaoweza kujuta kuendelea kubaki Arsenal baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Katika dirisha la usajili lilofungwa hivi karibuni kulikuwa na mengi sana yaliyojadiliwa kuhusiana na uhamisho wa wachezaji katika klabu mbalimbali za soka huko ulaya. Kwa Arsenal habari kuu ilikuwa kwa wachezaji waliondoka na waliosajiliwa wapya, lakini pia tusisahau wachezaji walibakia na klabu ya Arsenal.

Wakati Jack Wilshere akiruhusiwa kwenda Bournemouth kwa mkopo  katika kile inachoaminika ni kutafuta nafasi ya kushiriki zaidi katika soka, ndivyo ilivyokuwa kwa wenzake kama Calum Chambers aliyejiunga na klabu ya Middlesbrough siku iliyopita na Serge Gnabry aliyeuzwa moja kwa moja kwenda Werder Bremen ya Ujerumani. 

Pamoja na hayo Arsene Wenger aliamua kuwabakisha kikosini wachezaji kadhaa ambao yeye anaamini wanaweza kupambana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza msimu huu.

Wafuatao ni wachezaji watano ambao wanaweza kunufaika kwa kubakia na Arsenal au
 kujutia ni kwanini hawakuondoka kwenda kujiunga na klabu nyingine:

1. Mathieu Debuchy

Beki huyu wa kulia kutokea taifa la Ufaransa, anakabiliwa na msimu mwingine kwa kutumika kama mchezaji mbadala kwa Hector Bellerin(Umri: 21) baada ya kushindwa kujadiliana na uongozi wake kuhusiana na suala la yeye kuondoka Arsenal msimu huu. 

Debuchy alijiunga kwa mkopo na klabu ya Bordeaux Januari ili kusaka namba katika kikosi cha Ufaransa Euro 2016, na kujikuta akiwa nje kwa sababu ya majeruhi. Hiyo inaweza kuwa sababu iliyokatisha mipango ya klabu nyingine ambazo zilikuwa na nia na uwezo wa kumsajili beki huyo.

2. Kieran Gibbs

Kama ilivyo kwa Debuchy, Gibbs anajikuta akibakia chaguo la pili baada ya Nacho Monreal, na uwezekano wa yeye kupata nafasi ya uhakika katika timu yake ya taifa ya Uingereza pengine ingeongezeka endapo kama angeamua kuachana Arsenal na kujiunga na klabu nyingine ya Ligi Kuu. 

Lakini kuondoka kwake kwenda klabu nyingine akibakia kuwa vigumu, kwani Monreal angebakia bila mbadala, na ndio chaguo pekee la hakika Arsene Wenger pale Monreal anapokuwa na tatizo.

3. Chuba Akpom

Mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 20 aliyetumikia msimu mzima uliopita kwa mkopo katika klabu ya Hull City, ambaye pia alifanikiwa konga hisia za mashabiki wengi wa Arsenal katika mashindano ya pre-season kwa kufunga mabao manne anabakia na nafasi ndogo sana ya kuweza kufit katika mipango ya Arsene Wenger baada ya kuwasili kwa mshambuliaji matata kutokea klabu ya Deportivo ya Spain wiki hii, Lucas Perez kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 17m.

4. Yaya Sanogo

Maisha ya baadaye ya Sanogo katika klabu ya Arsenal bado ni ndoto na hali imekuwa mbaya zaidi baada ya majeruhi yake ambayo yalimfanya aendelea kuwa nje kwa muda mrefu. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipangwa moja kwa moja katika kikosi cha kwanza baada ya kusajiliwa na Arsenal mwaka 2013.

Maendeleo ya Sanogo yakaonekana kuwa mabaya tangu ulipoanza mlolongo wa kuhusishwa kuhamishwa kwa mkopo kuelekea klabu mbali mbali na uhamisho kushindikana huku hali yake kimchezo(majeruhi) ikidaiwa kuwa chanzo cha tatizo hilo. Kadri muda unavozidi kwenda na ndivyo nafasi yake kupangwa mara kwa mara katika kikosi cha Arsenal inavozidi kuwa ndogo.

5. David Ospina

Golikipa huyu wa taifa la Colombia alikuwa akihusishwa na mpango wa kuihama Arsenal baada ya kupoteza nafasi yake kwa Peter Cech, lakini Arsene Wenger amefanikiwa kumubakiza mchezaji huyu katika klabu ya Arsenal kutokana na sababu mbali mbali ikawamo na ya thamani yake kuwa kubwa bado. 

Wakati Cech bado anaumuhimu mkubwa klabuni na mwenye kuwapa matumaini makubwa Arsenal ya kushinda Ligi Kuu, kwa uzoefu wake wa kimataifa na vile vile kama mbadala pengine kumsaidia Wenger kuwatia moyo wachezaji wa Arsenal. 

Swali linakuja, ni kwa muda gani Ospina ataendela kuwa na furaha huku ameketi kwenye benchi na mwenzake akiwa golini? Wenger alijaribu kumtumia Ospina katika mashindano ya vikikombe mbali mbali msimu uliopita - ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa - lakini aliamua kumrejesha Cech baada ya makosa makubwa aliyoyafanya wakati Arsenal ikicheza dhidi ya Olympiakos.

Source: ESPN Soccer
ZeroDegree.
Wachezaji watano wanaoweza kujuta kuendelea kubaki Arsenal baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Wachezaji watano wanaoweza kujuta kuendelea kubaki Arsenal baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Reviewed by Zero Degree on 9/02/2016 12:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.