Loading...

Ngasa kavunja mkataba wake na klabu ya Afrika kusini, ..sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa mchezaji wa Toto Africans, Kagera, Yanga, Azam na Simba Mrisho Khalfan Ngassa ametangaza kuvunja mkataba wake na klabu ya Free state ya Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa barua ambayo inaonesha kuwa Ngassa kwa sasa ni mchezaji huru na anaruhusiwa kucheza katika klabu yoyote, imeeleza kwa ufupi kuwa Ngassa amevunja mkataba na Free State toka August 25 2016.

Mrisho Ngassa alijiunga na Free State kwa mkataba wa miaka minne baada ya kuondoka Yanga kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu wa 2014/2015 na amedumu nayo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Sababu kubwa iliyompelekea Kiungo huyo mpaka kuvunja mkataba wake ikidaiwa kuwa ni ukame wa mataji, ikiwa yeye ni mchezaji aliyezoea mafanikio lakini kwa upande wa Klabu ya Free State hapambani ipasavyo katika kuwania mataji.

ZeroDegree.
Ngasa kavunja mkataba wake na klabu ya Afrika kusini, ..sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote. Ngasa kavunja mkataba wake na klabu ya Afrika kusini, ..sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote. Reviewed by Zero Degree on 9/02/2016 11:08:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.