Loading...

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 awamu ya pili mwaka 2016



Ofisi ya Rais -TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016.

Wanafunzi 3,918 wamechaguliwa. Ambapo 2,413 ikiwa ni wasichana na 1,505 ikiwa ni wavulana, wote hao wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.


Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye ukurasa huu: www.tamisemi.go.tz 

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI.

Kuyaona majina hayo kwa urahisi bofya katika viunganishi vifuatavyo hapo chini:

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 awamu ya pili mwaka 2016 Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 awamu ya pili mwaka 2016 Reviewed by Zero Degree on 9/02/2016 10:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.