Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi mwaka 2017
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.
Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.
Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.
Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.
Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.
"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi mwaka 2017
Reviewed by Zero Degree
on
6/10/2017 09:37:00 AM
Rating: