Wananchi wa Tanga wamsubiri kwa shauku Dkt. Samia Suluhu
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuinadi sera ya Chama Chake pamoja na kuomba kura kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni muendelezo wa Kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025.
Dkt. Samia anatarajiwa kuwa na Kampeni zake kwenye Wilaya za Handeni, Pangani, Muheza, Korogwe na Tanga Mjini, akifanya Mikutano ya hadhara kwaajili ya kuwaeleza wananchi yaliyomo kwenye Ilani ya CCM ya 2025/30 sambamba na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2030.
"Wananchi tunaoishi kwenye Mkoa wa Tanga tutegemee maendeleo zaidi kwasababu Dkt. Samia ndiye Mgombea pekee ambaye aliahidi kupitia Ilani ya CCM na akatekeleza kwahiyo tunakwenda kuendelea na tunaamini wananchi watakiunga Mkono Chama chetu na watampa kura nyingi za Urais Mgombea wetu kwasababu amejipambanua katika kulinda amani ya nchi yetu lakini katika miradi ya maendeleo kazi kubwa imefanyika." Amesema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Rajab Abdulrahman.
Wananchi wa Tanga wamsubiri kwa shauku Dkt. Samia Suluhu
Reviewed by Zero Degree
on
9/28/2025 07:44:00 PM
Rating:
