Loading...

Griezmann aeleza kwanini hatokaa, akubali kujiunga na klabu ya Arsenal tena

Mshambuliaji wa Klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann
Nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann ameeleza sababu ya kwanini hatokaa akubali kujiunga na klabu ya Arsenal hata siku moja, baada ya klabu hiyo kushindwa kumsajili awali kabla hajajiunga na Atletico.

Katika chapisho lake jipya, Mfaransa huyo anasimulia jinsi Arsene Wenger alivyojaribu kumsajili mwaka 2013 alivyokuwa Real Sociedad.

Baada ya kuarifiwa na msuka mipango ya usajili wa Arsenal, 
Gilles Grimandi kwamba klabu yake inamhitaji, Griezmann alimwambia aliyekuwa mshauri wake, Bw Eric Olhats “Kuweka kando ofa zote nyingine zilizokuwa mezani”.

Hata hivyo, alishuhudia soko la usajili wa wachezaji likifungwa, wakati yeye akisubiri na hatimaye Arsenal ikamsajili Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.

Griezmann
“Nilisubiri, nikasubiri, na nikasubiri zaidi...ilipokuwa kimya, Eric alimpigia simu Grimandi, ambaye alisema kwamba, meneja bado ananihitaji na niendelee kusubiri.” alisema Griezmann kwenye kitabu chake.

“Hatimaye muda mfupi tu kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, akatujulisha kwamba Arsenal hataiweza kunisajili tena.”

“Sipendelei kuambiwa jambo fulani na lisitekelezwe, hivyo Eric alivyoniambia baadaye kwamba klabu hiyo ya London inanihitaji tena nilimwambia aachane nao

Mwaka uliofuata, Griezmann aliichezea timu yake ya taifa na kusani mkataba na klabu ya Atletico Madirid kwa paundi milioni 30, ambako ndio alifanikiwa kukuza jina lake zaidi.

Kwa sasa thamani yake ni karibia mara tatu ya ile ya awali na mashabiki wa Arsenal watakuwa wanashangaa uamuzi wa klabu yao kuacha kumsajili raia huyo wa Ufaransa, kufuatia nukuu kadhaa zinazodai kwamba hakuna nafasi kwa Arsenal kuweza kumsajili nyota huyo tena.
Griezmann aeleza kwanini hatokaa, akubali kujiunga na klabu ya Arsenal tena Griezmann aeleza kwanini hatokaa, akubali kujiunga na klabu ya Arsenal tena Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.