Loading...

Mama Wema atinga Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu

Mama Wema akiwa na Tundu Lissu
Mama Mzazi wa msanii wa filamu Bongo na Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu, Miriam ameenda Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapata matibabu nchini huyo.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amekuwa akitibiwa Nairobi tangu aliposhambuliwa kwa kupigwa risasi Septemba mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wa serikali na wa chama hicho wamekuwa wakienda kumjulia hali na sasa Mama wa Wema Sepetu amefanya hivyo.

Jana Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu, alimtembelea Lissu hospitalini hapo. Mama Wema na wanaye Februari 24 mwaka huu walitangaza kujiunga na Chadema.
Mama Wema atinga Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu Mama Wema atinga Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu Reviewed by Zero Degree on 11/29/2017 11:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.