Loading...

Dirisha la Usajili nchini Italia lafanyiwa mabadiliko


Dirisha la Usajili nchini Italia kwenye majira ya joto litafungwa Tarehe 18 Agosti, 2018 mwaka huu, siku moja kabla ya msimu mpya wa Serie A kuanza.

Uamuzi huo unafuata mfano wa Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo klabu ziliamua mnamo mwezi September kurudisha siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili hadi tarehe 9 mwezi Agosti kwenye majira ya  joto, kabla msimu mpya haujaanza.

Kamishina wa Serie A, Giovanni Malago pia alisema kwamba dirisha dogo la usajili katika kipindi cha baridi litafungwa kabla michuano ya 'championship' nchini humo haijarejea tarehe 20 Januari kufuatia mapumziko.

Malago alisema kwamba Ligi itapanga ratiba tarehe 26 Desemba na inaweza kupanga raundi mbili za mechi kati Krismas na Mwaka mpya, kama vile ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza. Hata hivyo, kutakuwa na wiki tatu za mapumziko.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports, Malago alisema: "Msimu ujao, mechi zitachezwa Desemba 22, 26 na 29 na championship itarejea Januari 20."
Dirisha la Usajili nchini Italia lafanyiwa mabadiliko Dirisha la Usajili nchini Italia lafanyiwa mabadiliko Reviewed by Zero Degree on 3/07/2018 12:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.