Loading...

Masau Bwire awabatiza Stand United jina jipya


Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapiga debe wa Stand United kutoka mkoani Shinyanga, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewabatiza jina jipya wapinzani wake.

Bwire ameamua kuwabatiza jina jipya Stand kufuatia kupoteza alama tatu muhimu jana kwa kuwaita kuwa ni wapiga POPO kutokana na aina ya upinzani waliouonesha.

Msemaji huyo ameamua kuwabatiza jina jipya Stand United huku akijigamba kuwa wao wapo kwa ajili ya kupapasa akieleza hawana utani hivi sasa.

Kikosi hicho cha Ruvu Shooting jana kimejiongeza pointi tatu muhimu kwa kufikisha 33 kwenye nafasi ya 7.

Stand wameendelea kusalia katika nafasi yao ya 9 wakiwa na pointi 32 huku wakiwa wamecheza michezo 27 msimu huu.
Masau Bwire awabatiza Stand United jina jipya Masau Bwire awabatiza Stand United jina jipya Reviewed by Zero Degree on 5/15/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.