Loading...

Nyota Arsenal asistiza kuwa hana mpango wa kuondoka Emirates

Wachezaji wa klabu ya Arsenal katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Uingereza
Hector Bellerin alianza kung'ara akiwa na Arsenal mwaka 2015 na tangu hapo amekuwa chaguo la kwanza la klabu hiyo katika nafasi ya beki wa kulia. Alianza maisha yake ya soka katika timu ya vijana ya Barcelona kabla hajajiunga na 'the Gunners' mwaka 2011.

Mhispania huyo amekuwa mchezaji tegemezi katika klabu hiyo msimu huu, akifanikiwa kucheza mechi 34 Ligi Kuu ya Uingereza. Lakini amepitia wakati mgumu katika siku za hivi karibunu baada ya kiwango chake kuonekana kushuka ukilinganisha na hapo nyuma.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na kuondoka Emirates, huku iliyokuwa klabu yake ya zamani, Barcelona, Real Madrid, Manchester United na Juventus zikiwa miongoni mwa klabu zinazohitaji saini yake.

Hector Bellerin
Lakini Bellerin anasistiza kuwa hana nia ya kuondoka Arsenal kwenye majira ya joto na ataripoti katika klabu hiyo kwenye maandalizi ya msimu ujao baada ya Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa taaifa ya Sky Sports, Bellerini alisema: “Nina mkataba mrefu, nimekuwa hapa London kwa muda mrefu sana, hapa ndio nyumbani kwangu kwa sasa.”

“Hakuna kitu kingine cha zaidi ninachokifikiria, kwenye majira ya joto. Tuna Kombe la Dunia mbele yetu, sijui kama nitaitwa au la, hilo ni suala la kusubiria tuone itakavyokuwa.

“Kama nitapewa nafasi, nitafurahi sana. Ukiachana na hilo, nina uhakika kwamba nitarejea hapa kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.”
Nyota Arsenal asistiza kuwa hana mpango wa kuondoka Emirates Nyota Arsenal asistiza kuwa hana mpango wa kuondoka Emirates Reviewed by Zero Degree on 5/12/2018 04:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.