Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 15 Mei, 2018

Marco Verratti
Juventus wanataka kumrejesha Marco Verratti nchini Italia kutokea Ufaransa, kama sehemu ya mkakati wao wa kusajili angalau kiungo moja mwenye uwezo mkubwa. (Corriere dello Sport)

Arsenal inaendeleza nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Nice, Jean-Michael Seri.

Everton wameanzisha mazungumzo na Monaco juu ya uhamisho wa kiungo mkabaji wa klabu hiyo ya Ufaransa, Kevin N'Doram. (L'Equipe)
  
Nyota ambaye anawindwa na klabu ya Arsenal, Julian Nagelsmann hataondoka Hoffenheim kenye majira ya joto, kwa mujibu wa mkurugenzi wa klabu hiyo.

Joachim Low ameongeza mkataba wake na timu ya taifa ya Ujerumani hadi baada ya Kombe la Dunia mwaka 2022. (Sky Sports)

Sam Allardyce atafukuzwa kazi katika klabu ya Everton ndani ya masaa 48 yajayo na Marco Silva ameibuka na kuwa chaguo la kwanza kuchukuwa nafasi yake.

West Ham wanataka meneja wa newcastle, Rafa Benitez achukue nafasi ya David Moyes.

Spurs wataanza kusikiliza ofa kwa ajili ya uhamisho wa Toby Alderweireld na Danny Rose kuelekea dirisha la usajili kwenye majira ya joto. (Mirror)

Petr Cech
Petr Cech ameionya Arsenal kwamba inaweza kujikuta inaingia miongoni mwa vilabu vinavyoajiri na kufukuza wakufunzi mara kwa mara kufuatia kuondoka kwa Arsene Wenger.

Arsenal wako tayari kujaribu bahati yao kwa mpa kibarua Mikel Arteta kama meneja mpya.

Fabio Coentrao amejitoa kwenye nafasi ya kuweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kwenye Kombe la Dunia - akidai kuwa amechoka sana hivyo itakuwa ni vigumu kwake kushiriki michuano hiyo.

Beki wa kati wa klabu ya Liverpool, Dejan Lovren amewaambia wapinzani wa vijana hao wa Anfield kuwa pesa sio kigezo cha kupata mafanikio.

Jorge Sampaoli ametangaza kikosi chake cha awali cha wachezaji 35 wa timu ya taifa ya Argentina kitakachoshiriki Kombe la Dunia - lakini hakutoa nafasi kwa nyota wa Tottenham, Erik Lamela.

Ryan Shawcross anataka Stoke City wachukue uamuzi wa haraka juu ya hatima ya meneja Paul Lambert.

Beki wa klabu ya Swansea, Angel Rangel analengwa na klabu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), DC United. (Sun)

Paul Pogba ana matumaini ya kuiongoza Ufaransa kupata mafanikio makubwa kwenye Kombe la Dunia.

Massimiliano Allegri
Massimiliano Allegri bado anaweza kuwa meneja mpya wa Arsenal. (Star)

Mauricio Pochettino amemwambia mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy kwamba anataka pauni milioni 100 kwa ajili ya kununua wachezaji wapya kwenye majira ya joto - pamoja na pesa yoyote itakayopatikana kwa kuuza wachezaji wao. (Express)

Steve Bould anachelewa kufanya uamuzi wa kama atabaki au kuondoka Arsenal, akisubiria kuona ni nani atateuliwa kuwa meneja mpya wa klabu hiyo baada ya Mikel Arteta kupewa nafasi kubwa.

Petr Cech anaamini Arsenal ina kikosi kinachoweza kushindania ubingwa msimu ujao bila kujali ni nani atakayeteuliwa na klabu hiyo kuchuwa nafasi ya Arsene Wenger. (Telegraph)

Klabu ya Tottenham imebakiwa na mwezi mmoja kuliambia Shirikisho la Soka Uingereza (FA) kama itaongeza mkataba wao wa miezi 12 katika Uwanja wa  Wembley.

Jose Mourinho anafikiria kumpa nafasi Kieran McKenna, mkufunzi wa timu ya Manchester United U18, kuwa mkuu wa benchi la ufundi linalofanya kazi nje ya uwanja kutokana na sintofahamu ya hatima ya Rui Faria. (Times)

West Ham hawajapoteza muda wowote kwenye kumsaka mrithi wa David Moyes baada ya kukutana na meneja wa Shakhtar Donetsk, Paulo Fonseca Jumatatu.

Sofiane Boufal amezungumzia uwepo wa uwezekano wa kurejea nchini Ufaransa kufuatia mgogoro wake na Mark Hughes, huku Southampton ililenga kumsajili winga wa klabu ya Celta Vigo, Pione Sisto anayekadiriwa kuwa na thamani ya karibu pauni milioni 36.

Matthew Bondswell
Manchester United wako kwenye mazungumzo na Nottingham Forest, juu ya uhamisho wa beki wa kushota wa klabu hiyo, Matthew Bondswell, 16. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 15 Mei, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 15 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/15/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.