Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 16 Mei, 2018

Messi na Neymar Jr, Barcelona
Lionel Messi amesema kuwa itakuwa ni pigo kubwa sana kwake kama aliyekuwa mchezaji mwenzake katika klabu ya Barcelona, Neymar Jr atajiunga na Real Madrid.

Diego Maradona amepewa kibarua cha Ukurugenzi katika klabu ya Dinamo Brest ya Belarus. (ESPN)

Mauricio Pochettino yuko tayari kuitolea nje Chelsea ili aendelee kuwa mzalendo kwa Tottenham.

Bodi ya Arsenal bado haijapitisa uteuzi wa Mikel Arteta kuwa mrithi wa Arsene Wenger. (Star)

Eden Hazard amesema kwamba, anafurahia kuwa na Chelsea lakini ametoa changamoto kwa klabu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wapya watakao kuwa na tamaa ya kushindania mataji.

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere ameachwa nje kwenye kikosi cha Uingereza kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi.

Meneja mpya wa timu ya taifa ya Italia, Roberto Manchin amesema kuwa atazungumza na Mario Balotelli kuhusiana na kurejea kikosini. 

Vigogo wa klabu ya Arsenal wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa Nice, Jean Michael-Serri. (Sky Sports)

Romelu Lukaku
Romelu Lukaku atakuwa fit kuanza na kikosi cha kwanza cha Manchester United siku ya Jumamosi kwenye fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea.

Atletico Madrid watamchunguza Kieran Tierney kwemye fainali ya Kombe la Shirikisho nchini Scotland na kujiunga na mbio za kuwania saini ya beki huyo wa Celtic.

West Ham wanataka golikipa wa Uingereza, Tom Heaton achukue nafasi ya Joe Hart msimu ujao. (Sun)

Lionel Messi amekiri kuhofia kumuona Neymar ndani ya jezi ya klabu ya Real Madrid.

Joe Hart amekasika baada ya kuamini kuwa meneja wake, David Moyes ndiye aliyemsababishia kukosa nafasi kwenye Kombe la Dunia.

Chelsea wamepewa siku saba kuhakikisha wanamshawishi Maurizio Sarri kutua Stamford Bridge - zaidi ya hapo watakabiliwa na ongezeko kubwa la bei.

Mikel Arteta anaweza kuingia kiulaini kwenye kibarua cha kuinoa Arsenal kufuatia baadhi ya wapinzani wake kuanza kujitoa kwenye mbio hizo.

Lionel Messi amesistiza kwamba bado hajawahi kufikiria kuondoka katika klabu ya Barcelona. (Mirror)

Patrick Roberts
Leicester na West Ham zitazajiribu kumsajili Patrick Roberts, ambaye anachezea Celtic kwa mkopo toka Man City baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho nchini Scotland. 

Stephen Thompson anakaribia kuuza kiasi kikubwa cha hisa zake za umiliki katika klabu ya Dundee United kwa muwekezaji kutoka America. (Express)

Arsenal wanakaribia kumteua Mikel Arteta kuwa meneja wao mpya.

Everton, Newcastle na Huddersfield ni miongoni mwa vilabu vinavyowania saini ya raia wa Kosovo, Donis Avdijaj anayeichezea klabu ya Roda ya Uholanzi kwa mkopo kutoka Schalke 04.

Swansea wanatarajia kukamilisha dili lao jipya la kwanza katika enzi mpya kwa kumsajili kiungo wa klabu ya Liverpool, Yan Dhanda kwa pauni 100,000. (Daily Mail)

Danny Rose ameishauri Spurs imuunge mkono Mauricio Pochettino kwenye mbio za kuwania Taji la Ligi Kuu ya Uingereza.

Hatima ya Paul Lambert kama meneja wa Stoke City bado hajulikani, kuelekea mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo wiki hii. (Telegraph)

Manchester United na Liverpool wanatarajiwa kualikwa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu litakaloshirikisha timu 24, ambayo itaviingizia vilabu hivyo faida ya zaidi ya pauni milioni 100. (Times)

Mikel Arteta
Mikel Arteta anakaribia kuwa meneja wa Arsenal, huku aliyekuwa mchezaji mwenzake wa Arsenal, Santi Cazorla akitarajiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 16 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 16 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/16/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.