Loading...

Wachezaji wa Yanga watakaoikosa Rayon Sports leo


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa na kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo Jumatano dhidi ya Rayon Sports, wachezaji kadhaa ikiwemo nyota wataukosa mchezo huo.

Yanga inashuka dimbani kucheza mechi hiyo ya pili katika hatua ya makundi ikiwa na kumbukumbu mbaya za kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger wa mabao 4-0 huko Algiers, Algeria.

Uhakika wa wachezaji ambao watakosekana kwenye mtanange huo ni Amis Tambwe ambaye bado hajaimarika vizuri kiafya, Donald Ngoma pia Beno Kakolanya ambaye alijitonesha goti lake katika mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbali na hao yupo Ibrahim Ajibu aliye na matatizo ya kifamilia, Papy Kambamba Tshishimbi aliyesafiri kurejea kwao kutokana na matatizo ya kiafya kwa ajili ya matibabu.

Wakati huo mchezaji Said Makapu atakuwa nje ya dimba kutokana na adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano zitakazomfanya awakose Rayon Sports.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 1 usiku ili kuwapa nafasi wafanyakazi kupata fursa ya kwenda kuutazam mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga watakaoikosa Rayon Sports leo Wachezaji wa Yanga watakaoikosa Rayon Sports leo Reviewed by Zero Degree on 5/16/2018 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.