Bobi Wine yamkuta tena
Bobi amebaniwa kufanya shoo na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Uganda (FUFA). Kupitia mitandao ya kijamii, Bobi amelaumu Serikali yake kwa kumuonea.“Ni kwa vipi wamekuwa wakinizuia? Ni kwa sababu Bobi Wine anahusika! Najua kuwa wanatumia kila mbinu kuzuia biashara zangu na vyanzo vya kupata chochote kitu,” aliandika Bobi Wine na kuongeza:
“Unajua kwa nini? Leo nimepokea barua wamezuia shoo yangu. Sababu? Wanadai eti wamepata oda kutoka FUFA. Hebu angalieni uwanja huohuo unafanya matamasha mengi na hawajawahi kuzuia,” alilalama Bobi.
Miezi michache iliyopita, Bobi na wabunge wengine kadhaa walikamatwa na Polisi wa nchini humo baada ya waandamanaji kupiga mawe gari la Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi. Katika kushikiliwa huko, ilidaiwa Bobi alipitia katika mateso makali.

Reviewed by Zero Degree
on
10/26/2018 07:50:00 AM
Rating: