Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Octoba, 2018

Toni Kross
Paris Saint-Germain wanamfuatilia kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, Toni Kross. (Mundo Deportivo)

Juventus imetoa ofa ya mkataba mpya kwa beki wa klabu hiyo, Aalex Sandro lakini Mbrazil huyo bado hajakubali vigezo na masharti ya mkataba huo hadi hivi sasa. (Calciomercato)

Tottenham wanatarajia kuipiku Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa klabu ya Atalanta, Miguel Almiron.

Mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 29,yoko tayari kuondoka Manchester United mwezi januari na amejipanga kuhamia Paris St-Germain.

Tottenham inavutiwa na golikipa wa Burnley na England Nick Pope, 26.

Mchezaji wa Manchester United Ashley Young, 33, anataka mkataba mpya wa miaka miwili na timu yake. (Mirror)

Manchester United inahofia kumpoteza golikipa wake, David de Gea kwa klabu ya Juventus, atakapokwenda kama mchezaji huru wakati mkataba wake na mashetani hao wa Old Traford utakapoisha.

Osmane Dembele aliondolewa kwenye kikosi cha Barcelona kilichocheza dhidi ya Inter Milan baada ya kuchelewa kikao cha kabla ya mechi kwa dakika 25.

Sandro Tonali
Chelsea inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Juventus kwenye msako wa saini ya kiungo wa klabu ya Brescia, Sandro Tonali, 18.
 
Mshambuliaji wa ufaransa Anthony Martial, 22, amekaukataa mkataba mpya ambao amepewa na timu ya Manchester United lakini mazungumzo ya makubaliano yanaendelea.

Real Madrid wanafanya jaribio lao la mwisho kumfanya Maurcio Pochettino kuwa meneja wao mpya, huku Julen Lopetegui akiendelea kuwa na wakati mgumu Santiago Bernabeu. 

Kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28,ambaye Ajax inamuwania, yuko tayari kuwa na timu ya Manchester City kwa muda mrefu kwa siku za usoni na kusaini mkataba mpya. 

Beki wa Kati wa Chelsea Gary Cahill, 32,amekubali kubaki katika timu yake licha ya kuwa kabla alisema anaweza kuondoka mwezi Januari. (Sun)

Mchezaji wa Chelsea kutoka Nigeria Victor Moses, 27 anaona kuwa hapo baadae atakosa muda wa kutosha wa kucheza. (Evening Standard)

Ipswich Town anamuona kuwa Paul Lambert ndiye atakuwa meneja wao baada ya kufukuzwa kwa Paul Hurst. (Independent)

Chelsea imesisitiza kuwa Roman Abramovich hana nia ya kuiuza klabu hiyo, licha ya kuenea kwa taarifa zinazodai klabu hiyo itauzwa kwa tajiri wa Cech, Petr Kellner.

Alexis Sanchez
Nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez ana matumaini klabu ya PSG itamsajili mwezi Januari. 

Sam Vokes anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu ya Burnley. (Daily Mail)

Pocettino yambidi aitafakari ofa aliyopewa na klabu ya Real Madrid - Sam Allardayce.

Ian Wright amewakosoa mashabiki wa Arsenal wanaomsema vibaya Hector Bellerin.

Sam Allardayce amemtaka Ruben Loftus-Cheek aondoke Chelsea ili aondokane na maumivu ya kusugua benchi. (talkSport)

Meneja wa klabu ya Leeds, Maarcelo Bielsa ana hamu kubwa ya kuungana kwa mara nyingine tena na nyota wa Athletic Bilbao, Ibai Gomez.

Chelsea ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya PSV Eindhoven, Hirving Lozano. (Star)

Crystal Palace itamrudisha meneja Roy Hodgson mwezi Januari katika dirisha la uhamisho ya orodha ya wafungaji ambayo alikuwa anaiwania.

Julen Lopetegui
Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez anataka kumfukuza meneja wa timu hiyo, Julen Lopetegui baada ya mechi ya El Clasico. (Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Octoba, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 26 Octoba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 10/26/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.