Loading...

Donald Trump avishambulia vyombo vya habari


Rais Donald Trump amevitaka vyombo vya habari kusitisha chuki isiyokuwa na kikomo baada ya kutoa taarifa ya kudhania kuwa vilipuzi vilikuwa vimetumwa kwa watu mashuhuri nchini Marekani.

Alizungumza hayo baada ya vifurushi hivyo kutumwa kwenye chombo cha habari cha CNN na viongozi wa juu wa chama cha Democrats ikiwajumuisha Barack Obama na Hillary Clinton.

Mpaka sasa hakuna kifurushi chochote kilicholipuka.

Shirika la ujasusi la FBI linawatafuta waliotuma mizigo hiyo.

Rais kukosoa jambo hilo linaonyesha ishara ya kutokuwa mkweli kwa sababu ni kawaida yake kutumia lugha zisizokuwa rafiki kwa vyombo vya habari na wapinzani wake.

Rais Trump alizungumza jana na kudai kuwa atahakikisha watu waliotuma vifurushi hivyo watakamatwa huku akiwataka vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli wowote.

Trump aliwataka watu kuwa watulivu na kusema matukio kama haya yanayohusisha masuala ya kisiasa yanapaswa kuisha na yasisababishe wanasiasa kutoelewana.

Mtu yeyote hapaswi kufananisha upinzani wa kisiasa na mashujaa wa kihistoria, jambo ambalo linafanyika mara kwa mara.

Hata hivyo rais Trump hakuweka wazi ni jambo gani ambalo amelenga kuwafanyia waliotuma mizigo hiyo.

Mapema Mkurugenzi wa shirika la habari la CNN Jeff Zucker alimkosoa rais Trump na katibu wa habari wa Ikulu ya white house kwa kutoelewa kuwa maneno yao yanaweza kuleta athari.

Hii inaonyesha wazi kabisa kuwa anakosa uelewa juu ya ubaya wa ongezeko la mashambulizi ya vyombo vya habari.

Zaidi bofya HAPA
Donald Trump avishambulia vyombo vya habari Donald Trump avishambulia vyombo vya habari Reviewed by Zero Degree on 10/25/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.