Loading...

Tanzania yapanda viwango vya soka FIFA


Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanda katika listi ya viwango vya soka vya dunia vya FIFA iliyotolewa hii leo, Alhamisi, Oktoba 25.


Katika viwango hivyo vilivyotolewa na FIFA, Taifa Stars imepanda nafasi nne zaidi hadi kufikia nafasi ya 136, kutoka nafasi ya 140 mwezi uliopita.

Taifa Stars ilicheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki ambayo ni ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwenye mapumziko ya kupisha michezo hiyo wiki mbili zilizopita.

Katika mchezo wa kwanza, Taifa Stars ilicheza ugenini na Cape Verde na kuambulia kichapo cha mabao 3-0, kabla ya mechi ya pili ya marudio kushinda kwa mabao 2-0 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ubelgiji imefanikiwa kuiondoa Ufaransa katika nafasi ya kwanza ya viwango vya soka vya dunia vya FIFA, huku Nigeria ikiongoza katika bara la Afrika, ikiwa katika nafasi ya 44.

Nchi za Afrika Mashariki zinaongozwa na Uganda iliyo katika nafasi ya 79, ikipanda nafasi nne zaidi katika mwezi huu. Kenya ikiwa katika nafasi ya 105, Rwanda katika nafasi ya 138 huku Burundi ikiwa katika nafasi ya 142.
Tanzania yapanda viwango vya soka FIFA Tanzania yapanda viwango vya soka FIFA Reviewed by Zero Degree on 10/25/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.