Loading...

Msuva aweka wazi siri ya mafanikio yake


KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa, Simon Msuva anayekipiga katika timu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, ametoa siri ya mafanikio yake kuwa amekuwa akitumia muda mwingi kujituma mazoezini.

Msuva alifanikiwa kuifungia timu ya taifa, Taifa Stars bao la kwanza katika mchezo dhidi ya Cape Verde kwenye ushindi wa mabao 2-0, mechi iliyochezwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msuva amesema kuwa amekuwa akitumia muda mwingi katika kujiimarisha mazoezini, hivyo kumfanya awe fiti kila kukicha.

“Siri ya mafaniko kwangu ni kutokana na kutumia muda mwingi kujiimarisha mazoezini kwa kujituma na ndiyo maana nimeweza kuwa hivi nilivyo.

“Hata katika timu yangu ya Difaa nimekuwa nikifanikiwa kufunga kutokana na kujitambua na kujituma, naona kitu cha kawaida kwangu kufunga, kocha amekuwa akinitegemea katika kikosi cha kwanza,” alisema Masuva.
Msuva aweka wazi siri ya mafanikio yake Msuva aweka wazi siri ya mafanikio yake Reviewed by Zero Degree on 10/19/2018 03:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.