Loading...

Prisons inamtaka straika huyu kutoka Simba SC


Kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohammed ‘Baresi’, amesema watazungumza na uongozi wa Simba kumwomba kwa mkopo straika wao wa zamani, Rashid Mohammed ‘Mo Rashid’, ili kuwaongezea nguvu katika safu ya ushambuliaji.

Prisons imeanza Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa haipo katika kiwango chake kutokana na kupata matokeo yasiyoridhisha na mechi ya juzi wametoka suluhu na Singida United.

Kwa mujibu wa taarifa ya BINGWA, Baresi, alisema wameanza kutafuta straika mwenye uwezo wa kutupia mabao huku wakijaribu kuwaomba Simba wawape Mo Rashid kipindi cha dirisha dogo kwa sababu anaonekana hana namba katika kikosi cha timu hiyo.

“Tatizo lililopo katika timu yangu ni safu ya ushambuliaji kushindwa kufunga mabao, tumeanza mchakato wakutafuta straika kwa usajili wa dirisha dogo, Simba wakikubali kutupa Mo Rashid kwa mkopo tutashukuru,” alisema Baresi.

Alifafanua kuwa hali wanayopitia kwa sasa ni ngumu kutokana na matokeo wanayopata kutowaridhisha watu wengi ila ameshabaini tatizo lililopo atalifanyia kazi kipindi cha dirisha dogo.
Prisons inamtaka straika huyu kutoka Simba SC Prisons inamtaka straika huyu kutoka Simba SC Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.