Loading...

Ammy Ninje ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi TFF


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemthibitisha Ammy Ninje (Pichani) kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo. Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Oscar Mirambo ambaye ataendelea na jukumu lake la Ofisa Maendeleo wa Soka la Vijana.

Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na umepata siku 60 za kutangazwa kabla ya kufanyika.

Aidha kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimepitisha mabadiliko madogo kwenye kamati ndogo ndogo za TFF. Mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na wengine kukabiliwa na majukumu mengi.

KAMATI YA NIDHAMU

1. Kiomoni Kibamba - Mwenyekiti
2. Peter Hella - M/Mkiti
3. Kassim Dau - Mjumbe
4. Handley Matwenga - Mjumbe
5. Twaha Mtengera - Mjumbe

KAMATI YA RUFAA MAADILI

1. Richard Mbaruku - Mwenyekiti
2. Thadeus Karua - M/Kiti
3. Mh. Mussa Zungu - Mjumbe
4. Asp Benedict Nyagabona - Mjumbe
5. Lugano Hosea - Mjumbe

KAMATI YA UCHAGUZI
1. Malangwe Ally - Mwenyekiti
2. Mh. Mohamed Mchengela - M/Kiti
3. Benjamini Karume - Mjumbe
4. Mohamed Gombati - Mjumbe
5. Hamisi Zayumba - Mjumbe
Ammy Ninje ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi TFF Ammy Ninje ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi TFF Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 12:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.