Loading...

Chirwa alitusumbua sana wakati tunamhitaji - Zahera


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekanusha taarifa za klabu hiyo kumrejesha kundini mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa ambaye aliondoka mwanzoni mwa msimu huu.

Chirwa ambaye aliichezea Yanga misimu miwili mfululizo, aliondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita akijiunga na klabu na Nagoon ya nchini Misri.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera
Kwa mujibu wa taarifa ya EATV, kocha Mwinyi Zahera amesema, "Taarifa hizo ni za uongo, Chirwa alitupatia matatizo sana wakati Yanga ilikuwa na uhitaji wake".

"Yeye aliiacha timu ina matatizo mengi, karibia mechi nne au tano alikataa kucheza kwasababu hawakumlipa mshahara na pia alitakataa kufanya mazoezi kwasababu ya pesa. Tulisafiri kwenda Morogoro na wachezaji wachache sana, yeye alikataa kusafiri na timu, mchezaji wa vile siwezi kumrudisha kwenye timu yangu", aliongeza.

Chirwa alionekana katika mchezo wa Yanga wa wikiendi iliyopita, mchezo ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Alliance katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Chirwa alitusumbua sana wakati tunamhitaji - Zahera Chirwa alitusumbua sana wakati tunamhitaji - Zahera Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.