Loading...

Ripoti ya MV Nyerere yatua kwa Waziri mkuu

Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.

Majaliwa amepokea ripoti hiyo leo, Alhamisi Oktoba 25, 2018 kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.

Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.

“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.” amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi.

MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa. Septemba 24, Waziri Mkuu alitangaza kamati ya kuchunguza ajali hiyo.
Ripoti ya MV Nyerere yatua kwa Waziri mkuu Ripoti ya MV Nyerere yatua kwa Waziri mkuu Reviewed by Zero Degree on 10/25/2018 05:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.