Loading...

SportPesa kumtajirisha bondia Mwakinyo

Akikabidhiwa mkataba huo
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya SportPesa Tanzania, leo imefanikiwa kutoa neema ya udhamini wa miaka mitatu kwa bondia Hassani Mwakinyo.

Katika miaka hiyo mitatu Mwakinyo ataitumikia SportPesa kama Balozi wake kwenye shughuli zake zote, ambapo ataivaa nembo hiyo katika mapambano yake yote atakayofanya ndani ya miaka hiyo.

Akizungumzia kuingia kwa mkataba huo Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas, alisema wao kama kampuni wanajisikia faraja kudhamini suala la ngumi kwani imekuwa desturi yao kuhakikisha wanadhamini mambo ya michezo kwa lengo la kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao.

Tarimba Abbas, Mwakyembe wakishuhudia ukamilisho wa mkataba huo na Mwakinyo
“Kudhamini vipaji kama hivi ni jambo la kawaida sasa kwetu kwani tulianza kudhamini kwenye masuala ya mpira na leo hii tunaingia rasmi kwenye ngumi, lengo likiwa ni kuhakikisha tunaimalisha michezo yote hapa nchini,” alisema.

Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amewapongeza Sportpesa kwa hatua hii huku akizitaka kampuni nyingine nchini kutoa udhamini katika michezo kama ilivyofanya SportPesa.

Picha ya pamoja
SportPesa kumtajirisha bondia Mwakinyo SportPesa kumtajirisha bondia Mwakinyo Reviewed by Zero Degree on 10/25/2018 06:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.