Loading...

Serikali yamfungia Wema Sepetu kwa muda usiojulikana

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo (kulia) Katibu muhtasi wa Wema Sepetu, Neema Ndepanya na Wema Sepetu (kushoto) akiwa amekata nywele
Bodi ya Filamu nchini, imemfungia muigizaji maarufu wa filamu mwanadada, Wema Sepetu kutojishughulisha na uigizaji kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake chafu zilizosambaa mtandaoni.

Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo amesema kuwa Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni na amekuwa akionywa na vyombo husika lakini amekuwa akirudia.

"Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii, na kwakuwa amekwisha onywa mara kadhaa safari hii tumeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu", amesema Fissoo.

Ameongeza kuwa "Kitendo kile kimelidharirisha taifa, jinsia na mashabiki wake wameiga tabia baadhi kupitia video ile, hivyo basi kwakuwa amekiri na kuomba radhi kwa maandishi, atatumikia adhabu hiyo mpaka pale tutakapojiridhisha kuwa amebadilika".

Mapema jana Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambapo ilimuonesha akiwa faragha na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.
Serikali yamfungia Wema Sepetu kwa muda usiojulikana Serikali yamfungia Wema Sepetu kwa muda usiojulikana Reviewed by Zero Degree on 10/26/2018 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.