Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 22 Octoba, 2018

Kiungo wa klabu ya Lyon, Nabil Fekir
Klabu ya Bayern Munich inalenga kumsajili nyota wa klabu ya Lyon, Nabil Fekir na mabingwa hao wa Ujerumani walimtuma skauti wao akamchunguze kiungo huyo kutoka Ufaransa. (Kicker)

Meneja Jose Mourinho anajaribu kuwashawishi maafisa wa Manchester United kufadhili mpango wa kumpata mlinzi bora zaidi ifikapo Januari. (Times)

Lionel Messi ameanza progarm maalumu ya mazoezi baada ya kuumia mkono kwenye mechi yao na Sevilla. 

Neymar alichochea tetesi zinazomhusisha na kurejea Hispania kwa kuutembela mji wa Barcelona wikendi iliyopita. (Marca)

Mourinho atafanya uchunguzi wa ndani kuhusu ni vipi orodha ya kikosi cha Manchester United ilifichuliwa kabla ya mechi ya Jumamosi iliyotoka sare na Chelsea. (Daily Mail)

Guti anatarajiwa kuchukua nafasi ya Julen Lopetegui Real Madrid kufuatia mabingwa hao wa UEFA kuwa na mwanzo mbaya msimu huu. (AS)

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, amekana kuwa na uhusiano mbaya na meneja Jose Mourinho. (Evening Standard)

Beki wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Marcelo anataka kumfuata Cristiano Ronaldo Juventus. (Tuttosport)

Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui anaripotiwa kukaribia kutimuliwa huku meneja wa kikosi cha B Santiago Solari akiwa katika nafasi ya kuchukua mahala pake. (Talksport)

Adrien Rabiot
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot, 23, ambaye amehusishwa na Liverpool na pia Juventus, anaripotiwa kukaribia kuongeza mkataba wake na klabu hiyo wa Ufaransa. (Calciomercato)

Borussia Dortmund, waliomchukua mchezaji wa miaka 18 Jadon Sancho kwenda Bundesliga wanamtazama lkiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, 18, mshambuliajia wa Chelsea Hudson-Odoi, 17, na mshambuliaji wa miaka 17 wa Liverpool Bobby Duncan. 

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Prince Mohammed bin Salman anatarajiwa kukutana na wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wiki chache zinazokuja, kuwasilisha ofa ya dola bilioni 4 kuinunua klabu hiyo.
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez, ambaye kikosi chake kiko chini katika jedwali la Premier League, anakiri kuwa anaishiwa na muda huko St James' Park. 

Manchester City wanakataa kubadilisha msimamo wao kuhusu masharti ya mkataba wake na Raheen Sterling, na kuongeza hofu kuwa mchezaji huyo wa miaka 23 wa England anaweza kuondoka msimu ujao. (Mirror)
Fiorentina wamewaambia Manchester United kuwa mlinzi raia wa Serbia Nikola Milenkovic, 21, atagharimu pauni milioni 40 ikiwa ni milioni 10 zaidi na wana moyo wa kutumia pesa kwa mchezaji huyo wa miaka 21.

Manchester City wanatathmini ofa ya pauni milioni 40 kwa mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 wa Uholanzi pia amehusishwa na Manchester United na Tottenham. (Sun)
Chelsea wanataka kumfanya Eden Hazard kuwa mchezaji anayelipwa kitita cha juu zaidi katika Ligi ya Uingereza kwa kumpa ofa ya mshahara wa dola 350.000 kwa wiki.

Anaweza kupigwa marufuku ya kuvuka laini na makabiliano na kocha wa pili wa Chelsea Marco Ianni huko Stamford Bridge.

Tottenham wanapanga kumuendea kiungo wa kati wa Blackburn, Bradley Dack, 24, kutokana na ripoti nzuri za majenti.

Real Madrid wako tayari kumpa ofa Sterling mwezi Januari. (Express)

Nikola Milenkovic
Meneja Manchester United Jose Mourinho anataka kumleta mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic. Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Serbia anawekewa thamani ya dola milioni 40 na klabu ya Italia kwa kuwa wanajua anawindwa na United, Tottenham, Chelsea, Arsenal na Juventus. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 22 Octoba, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 22 Octoba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 03:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.