Loading...

Wanariadha wa Tanzania washinda medali za dhahabu nchini Japan


WANARIADHA wa Tanzania, Marco Joseph, Fabian Joseph na Amina Mohamed wameibuka washindi wa medali za dhahabu katika mashindano ya riadha ya ‘Nagai Marathon’ yaliyofanyika nchini Japan.

Marco Joseph ameibuka na medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio ndefu za umbali wa takribani kilomita 42 huku Fabian Joesph na Amina Mohamed wakishinda katika mbio fupi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Jumapili iliyopita.

Akithibitisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja amesema,

“Washiriki zaidi ya 1000 walikuwepo hapo katika mashindano hayo, sisi tuliwakilishwa na washiriki 8 na kati yao, mmoja alipata matatizo ya misuli kwahiyo hakumaliza lakini wengine walifanya vizuri “.

“Kilomita 21 tumepata nafasi ya kwanza, pili na ya tatu, ambapo nafasi ya kwanza ni Amina Mohamed, ya pili ni Rosalia Fabian na ya tatu ni Silvia Masatu. Kwa wanaume, wa kwanza ni Fabian Joseph na nafasi ya pili ameshinda Wilbert Peter“, ameongeza.

Kwa upande wa mwanariadha, Marco Joseph amesema kuwa anajisikia furaha kwa kushinda medali hiyo huku aakiamini kuwa atashiriki mashindano ya Olympic yatakayofanyika mwaka 2020 nchini Japan.
Wanariadha wa Tanzania washinda medali za dhahabu nchini Japan Wanariadha wa Tanzania washinda medali za dhahabu nchini Japan Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.