Baraza halitasita kufuta matokeo ya wataokafanya udanganyifu - Msonde
Katibu Mkuu wa Baraza la Mtihani la Taifa, Dkt. Charles Msonde. |
Hayo yamesemwa leo Novemba 4, 2018 jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza hilo,Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandish wa habari ambapo ameeleza kuwa kitendo cha mtu ,mmiliki ,msimamizi au mwanafunzi kufanya vitendo vya udanganyifu ni kosa la jinai .
”Baraza halitasita kukifutia kituo cha kufanyia mtihani, kufuta matokeo kwa watu wataokafanya udanganyifu kwenye mtihani ikiwemo kuvujisha mtihani au kuingia na majibu kwenye vyumba vya kufanyia mtihani", amesema Msonde.
Dkt. Msonde ameongeza kuwa baraza linaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri wanafunzi katika kipindi chote cha miaka minne ya Elimu ya Sekondari hivyo matarajio yao ni kuwa wanafunzi watafanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mtihani.
Sambamba na hayo Dkt Msonde amebainisha kuwa jumla ya watahiniwa 427,181 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ,ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 368,227 na watahiniwa wa Kujitegemea ni 58,954 ambapo kati ya watahiniwa wa shule 368,227 waliosajiliwa ,wanaume ni 180908 sawa na. asilimia 49.13 na wanawake ni 187,319 sawa na asilimia 50.87.
Watahiniwa wenye mahitaji maalumu ni 562 kati yao 372 ni wenye uoni hafifu,44 ni wasioona,109 wenye ulemavu wa kusikia na 37 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili.

Reviewed by Zero Degree
on
11/04/2018 01:55:00 PM
Rating: