Loading...

Daktari feki aingia anga za Kamanda Muroto


JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassan Abdallah Athuman, umri miaka 38 kwa tuhuma za kujifanya Daktari wa magonjwa ya binadamu bila kuwa na vibali maalum.

Kamanda Gilles Muroto amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo November 24, 2018.

RPC Muroto amesema; “Huyu tumemkamata eneo la Kijiji cha Mwakisabe alikuwa akitoa Taaluma ya Utabibu bila ya kusomea ni Daktari feki, huyu aliwahi kukamatwa huko nyuma kwa kosa kama hili, alitorka Mahakamani.”
Daktari feki aingia anga za Kamanda Muroto Daktari feki aingia anga za Kamanda Muroto Reviewed by Zero Degree on 11/24/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.