Loading...

Dkt. Mengi kuanzisha kiwanda cha magari nchini


Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dk. Reginald Mengi leo ametia saini mkataba wa makubaliano baina ya IPP Automobile Ltd na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation ya Korea Kusini kwa ajili ya uanzishaji wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini kitakachoanza kazi mwakani.

Dk. Mengi amesema kuwa uwekezaji huo utagharimu dola za Mareklani milioni 10 sawa na shilingi bilioni 22 za Tanzania na kusema kuwa katika kipindi cha mwezi Oktoba mwakani gari la kwanza litatolewa katika kiwanda hicho cha IPP Automobile kitakachojengwa eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi.
"Kiwanda cha IPP Automobile Limited kwa kushirikiana na kampuni ya Youngsan Glonet Corporation (KOTA) kinatarajia kuunda magari aina ya Kia, Hyundai na Daewoo, ambapo kati ya September na October mwaka 2019 Tanzania itaanza kutumia gari la kwanza", amesema Dkt. Mengi.

Shughuli ya utiaji saini makubaliano hayo imefanyika Ofisi za Makao Makuu ya IPP Dar es Salaam ambapo, Dk. Mengi amesema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha magari 1,000 ya aina tatu na kutoa ajira rasmi kwa watu 500 na zisizo rasmi zaidi ya 1000.

Kwa upande wake balozi wa Korea nchini Tanzania Song Geum Young amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa sera ya Tanzania ya Viwanda na kuongeza kuwa kitasaidia kuongeza ajira pamoja na mapato kwa nchi.
Dkt. Mengi kuanzisha kiwanda cha magari nchini Dkt. Mengi kuanzisha kiwanda cha magari nchini Reviewed by Zero Degree on 11/20/2018 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.