Ibrahimovic anaweza kurejea katika klabu hii barani Ulaya
Zlatan Ibrahimovic anaweza kuwa mchezaji aliyeenda kutalii katika Ligi Kuu ya Marekani, MLS kwa msimu mmoja.
Baada ya kufikisha mabao 22, 'assist' 10 akiwa na LA Galaxy, Gazzetta Dello Sport imetoa ipoti inayodai kwamba Ibrahimovic anasubiia simu kutoka kwa mkurugenzi wa kandanda wa klabu ya AC Milan Leonardo, ikiambatana na ofa ya mkataba wa miaka sita na Milan mezani.
Ibrahimovic na Leonardo wana historia ya kufanya kazi pamoja – Leonardo alikuwa Paris Saint-Germain wakati Ibrahimovic anajiunga na klabu hiyo ya Ufaransa akitokea AC Milan, ambako Ibrahimovic alicheza kwa muda wa misimu miwili, kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa ameondolewa kwenye kipindi cha miezi 18 kutoka kuuguza mejeaha katika goti lake la kulia na hajaonyesha dalili za kuweza kuigaharimu timu yake kutokana na majeraha katika kipindi chote akiwa na Galaxy, ambako alifanikiwa kuanza na kikosi cha kwanza katika mechi 24 au 27 baada ya kujiunga na klabu hiyo mwezi Mei.
Ripoti kutoka nchini Italia zinasema kuwa Zlatan ainaweza kupata ongezeko la zaidi ya dola milioni 2.3 kwa muda wa miezi sita huko Milan, ambayo ni zaidi ya ya mshahara wake wa msimu mmoja nchini Marekani.
Kama hii itaweka ukomo wa muda wa Zlatan katika ligi kuu ya Marekani, MLS ataondoka akiwa amedhihirisha kwamba aliikamia vikali ligi hiyo lakini pia safu ya ulinzi ilivyokuwa mbovu katika klabu ya LA Galaxy mwaka 2018. Ni vigumu sana kwa timu yenye magoli 22 ya Ibrahimovic kushindwa kufuzu hatua ya mtoano.
Raia huyo wa Sweeden anajiunga na nyota kama Didier Drogba na Wayne Rooney kama mchezaji aliyetokea barani Ulaya hivi karibuni na kuonyesha uwezo wake katika MLS. Hata hivyo, Ibrahimovic haakumbukwa pamoja na wachezaji kama David Beckham, Robbie Keane, Thierry Henry na David Villa, ambao wote walikuwa na mikataba mirefu katika MLS na klabu zao.
Ibrahimovic anaweza kurejea katika klabu hii barani Ulaya
Reviewed by Zero Degree
on
11/20/2018 12:50:00 PM
Rating: