Fisi waongezeka Ngorongoro
Kwa mujibu wa taarifa ya Habari Leo, Kamishna wa hifadhi hiyo, Dk Fredy Manongi alisema baadhi ya wanyama walioathirika na ongezeko la fisi ni pamoja na duma ambao watoto wao huwa wanaliwa na fisi na kutishia kutoweka kwa wanyama hao ambao wamekuwa wakiwindwa na makundi makubwa ya fisi wenye njaa kali.
Alisema hivi sasa mamlaka hiyo inatekeleza mradi wa kudhibiti fisi ndani ya hifadhi hiyo, wakiona inafaa baada ya utafiti wa mradi huo watapunguza fisi hao ili kuwezesha hifadhi hiyo kuwa na fisi wachache kulingana na eneo la hifadhi hiyo. Kuhusu idadi ya simba, Kamishna Manongi alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna simba wapatao 1,172 ambao idadi yao haiongezeki kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia ujenzi wa mradi wa jengo la ghorofa 14 ambalo ni kitega uchumi cha mamlaka hiyo, alisema ni mradi mbadala wa kuiwezesha mamlaka hiyo kupata kitega uchumi kingine iwapo hifadhi itatetereka kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani pindi ukitokea tena na kuathiri sekta hiyo ya utalii.
Alisema gharama za awali za mradi huo ilikuwa ni Sh bilioni 42 kutokana na mabadiliko yaliyotokana na kupanda kwa bei ya gharama za vifaa vya ujenzi, gharama hiyo iliongezeka hadi kufikia Sh bilioni 45 na hadi sasa jumla ya Sh bilioni 39.4 zimeshalipwa kwa mkandarasi wa jengo hilo.
Akizungumzia mradi wa jengo hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) kulitangaza jengo lake la kitega uchumi lenye urefu wa zaidi ya ghorofa 10 lililopo katikati ya Jiji la Arusha ili liweze kupata wawekezaji, hivyo kuingizia mapato mamlaka hiyo .

Reviewed by Zero Degree
on
11/25/2018 02:50:00 PM
Rating: