Loading...

Hiki ndicho kiasi cha nyama unachotakiwa kula kwa mwaka


Ripoti ya shirika la Chakula duniani (FAO), imeeleza kuwa mtanzania anakula kilo 15 za nyama kwa mwaka kiasi ambacho ni cha chini sana ukilinganisha na mahitaji ya kiafya kwa mwanadamu.

Kupitia MJADALA wa East Africa Television, Novemba 5, 2018, Afisa nyama kutoka bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Edgar Mamboi amesema wastani wa kawaida wa kula nyama kwa mwanadamu ni kilo 50 kwa mwaka.

''Nyama ni muhimu kwa afya, sisi kama bodi ya nyama tunashirikiana na idara nyingine za afya pamoja na wadau kuhakikisha angalau elimu sahihi ya ulaji nyama inasambaa na kusaidia watanzania wengi kutumia nyama'', amesema.

Aidha Mamboi amesema Bodi ya nyama kwasasa ipo kwenye mchakato wa kuandaa mpango wa bei ya nyama jambo ambalo linashirikisha wauzaji wa nyama na idara nyingine ambapo bei maalum itasaidia kila mtu kuweza kununua nyama.

Mamboi amesisitiza kuwa kwa kawaida mwanadamu hawezi kufikisha kilo 50 kwa mwaka kwa kutegemea nyama katika mlo mmoja wa siku hivyo kuna ulazima wa kula nyama mara nyingi iwezekanavyo kwa siku.

Katika kuhitimisha afisa nyama huyo amesema kuna taarifa nyingi za upotoshaji juu ya aina gani ya nyama inafaa kuliwa kwa kuweka bayana kuwa nyama yoyote inafaa kwa afya ilimradi iive haijalishi iwe imechomwa, imekaangwa au kukaushwa.
Hiki ndicho kiasi cha nyama unachotakiwa kula kwa mwaka Hiki ndicho kiasi cha nyama unachotakiwa kula kwa mwaka Reviewed by Zero Degree on 11/06/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.