Kesi ya Halima Mdee kusikilizwa kwa siku mbili
Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba ameuagiza upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli, inayomkabili mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kuhakikisha wanapeleka mashahidi mahakamani ili iweze kumalizika ndani ya mwaka huu.
Hakimu Simba amesema hayo leo Novemba 21, baada ya upande huo kushindwa kuleta shahidi aliyepangwa kusikilizwa jana, lakini haikuweza kuendelea kutokana na maadhimisho ya siku ya Maulid ambayo kitaifa huwa ni mapumziko.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za kimahakama, kesi hiyo ilibidi iendelee siku inayofuata ambayo ni leo, lakini ikashindikana kutokana na shahidi kutofika, ambapo Hakimu Simba amepanga kesi hiyo kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, Disemba 10 na 11, wakati Mahakama itakaposikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.
Mdee ambaye analiongoza Jimbo la Kawe kwa kipindi cha pili mfululizo, alifikishwa mahakamani Julai 10, 2017 kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Rais na yupo nje kwa dhamana.
Upande wa mashtaka unadai kuwa Julai 3,2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka kuwa Rais Magufuli “anaongea hovyohovyo, anatakiwa afungwe breki”.
Upande huo unadai kuwa kitendo hicho kingeweza kusababisha kuvunjika kwa amani. Awali leo, wakili wa Serikali, Patrick Mwita aliieleza mahakama kuwa shahidi ambaye alitakiwa kutoa ushahidi wake, alitaarifiwa kuwa angefanya hiyo jana, hivyo hakuweza kufika leo.
Tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo wameshatoa ushahidi wao, akiwemo Batseba Kasanga, ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki.

Reviewed by Zero Degree
on
11/21/2018 02:35:00 PM
Rating: