Loading...

Kiwanda cha nguo kujengwa mkoani Simiyu

Rais wa chama cha wafanyabiashara Nchini Uturuki, Cengiz Ertas
Rais wa chama cha Wafanyabiashara Nchini Uturuki, Cengiz Ertas ameuhakikishia uongozi wa Mkoa wa Simiyu, kuwa watajenga na kuwekeza katika kiwanda kikubwa cha kutengeneza nguo Mkoani Simiyu.

Rais huyo ameyasema hayo leo wakati wa kikao chake na wafanyabiashara wa pamba Mkoani humo, ikiwa ni moja ya lengo kuu la kujionea mazingira na fursa za uwekezaji Mkoani humo.

Eartas amesema kuwa chama cha wafanyabiashara wa uturuki wako tayari kuwekeza katika kiwanda hicho cha nguo kutokana na uwepo wa malighafi za kutosha Mkoani humo.

Ameongeza kuwa watahakikisha ndani ya miezi mitatu mchakato wa uanzishwaji wa kiwanda hicho utakuwa umekamilika.

Pia amewaalika wafanyabiashara wa pamba Mkoani humo,katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara pamoja na mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony mtaka kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara wa uturuki ambao utafanyika january 2018.

Nae katibu wa chama cha wafanyabiashara wa pamba Mkoani Simiyu Boaz Ogola ameushukuru uongozi wa wafanyabiashara wa Uturuki kwa uamuzi wa kuja kuwekeza Mkoani Simiyu na kwamba kwao itawarahisishia gharama za kusafirisha pamba kwenda nje.
Kiwanda cha nguo kujengwa mkoani Simiyu Kiwanda cha nguo kujengwa mkoani Simiyu Reviewed by Zero Degree on 11/22/2018 05:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.