Loading...

Neymar, Kylian Mbappe wazua hofu PSG


Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya mchezo wa PSG dhidi ya Liverpool Ligi ya Mabingwa, vigogo hao wa Ufaransa wameingiwa na hofu ya majeruhi ya Neymar na Kylian Mbappe. Wachezaji wawili tegemezi katika kikosi cha PSG, wote wawili Neymar na Mbappe waliumia wakati wa michuano ya kimataifa.

Kylian Mbappe, Ufaransa
Kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Uruguay jijini Paris, Mbappe aliumia bega baada ya kuanguka mnamo dakika ya 36. Alitolewa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Florian Thauvin.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika meneja wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps alisema, “Mbappe ana uvimbe begani, alianguka vibaya sana. Itamlazimu kusubiri asubiri maelekezo kutoka kwa madaktari wetu. Natumaini halitakuwa jeraha baya sana.”

Neymar Jr, Brazil
Neymar alicheza dakika nane tu za mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Cameroon kabla hajaondoka uwanjani baada ya kuhisi maumivu ya misuli. Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar alisema kwamba jeraha la Neymar halitachukua muda mrefu kupona. 
Lasmar alisema, “Alitoka nje akilalamika anahsikia maumivu. Alijisikia vibaya, atahitaji muda wa kutosha kutathimini hali ya tataizo lake na kufanya vipimo, lakini tatizo lake sio kubwa saba.”

PSG wako nafasi ya tatu kwenye kundi lao la Ligi ya Mabingwa nyuma ya Napoli na Liverpool. Walipoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield. Hata hivyo, safasi hii wanapewa kipaumbele kwa kuwa watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Ingawa PSG ina wachezaji wazuri wakutosha katika kikosi chao, kukosekana kwa Neymar na Mbappe kwenye mchezo dhidi ya Liverpool litakuwa ni pigo kubwa sana kwao.

Kabla ya kuvaa Liverpool, PSG itacheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue dhidi ya klabu ya Toulouse siku ya Jumamosi.
Neymar, Kylian Mbappe wazua hofu PSG Neymar, Kylian Mbappe wazua hofu PSG Reviewed by Zero Degree on 11/22/2018 04:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.