Lugola awaondoa hofu mabalozi kuhusu usalama
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola akifanya mazungumzo na balozi wa kenya, dan kazungu. picha na mtandao
|
Akizungumza katika vikao na mabalozi hao waliofika ofisini kwake kwa nyakati tofauti jana, Lugola pia aliwaomba wawakilishi hao wa nchi zao nchini waendelee kushirikiana na wizara yake na nchi kwa ujumla.
Lugola aliwahakikishia mabalozi hao kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa wizara yake imejipanga kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi, nashukuru sana kwa kunitembelea. Najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote. Wizara yangu pamoja na nchi kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola alipozungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Thami Mseleku.
Kwa upande wake, Balozi Mseleku alisema akiwa nchini anajiona kuwa yuko nyumbani kwa sababu nchi yake ina historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania.
Balozi wa Italia, Roberto Mengoni, alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza wizara hiyo na pia alimhakikishia ushirikiano zaidi kati ya nchi yake na Tanzania.
Naye Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu, alisema Tanzania ni nchi yake na anajisikia furaha kuwapo nchini kwa sababu alishawahi kufanya kazi miaka kadhaa iliyopita nchini, hivyo nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala mbalimbali Tanzania.

Reviewed by Zero Degree
on
11/22/2018 10:05:00 AM
Rating: