Mayweather kuzipiga na Mjapan wa miaka 20
Mayweather hajawahi kupigana ndani ya MMA na ratiba ya pambano hilo na Nasukawa bado halijathibitishwa.
“Nilitaka kufanya kitu cha tofauti ,” alisema bingwa huyo mstaafu wa dunia wa uzito wa juu. “Nilitaka kuonyesha ujuzi wangu nje ya Marekani na niwe katika pambano maalumu. Ninataka kuwapa watu kile wanataka — damu, jasho na machozi.”
Bondia huyo mwenye miaka 41 alisema taratibu na daraja la uzito vitathibitishwa ndani ya wiki chache zijazo. Mabondia wote wawili wana rekodi nzuri katika michezo yao — Mayweather ameshinda mapambano 50-0 bila kupoteza ilhali Nasukawa ameshinda 27-0 bila kupoteza ndani ya masumbwi na 4-0 ndani ya MMA.
“Ni pambano kuu sana katika maisha yangu na ninataka kuwa mtu anayebadilisha historia. Nitafanya hivyo kwa kutumia viganja vyangu hivi, kwa pigo moja tu — tazameni mtaona,” alisema Nasukawa.
Mayweather hajawahi kupigana pambano lolote tangu astaafu na kumpiga Conor McGregor mwaka 2017 lakini amekuwa akihusishwa na mapambano kwa ajili ya pesa na mstaafu Manny Pacquiao.
Katika mahojiano yake na CNN’s Talk Asia hivi karibuni alisema, nafasi ya pambano lingine la marudiano na Pacquiao “ipo.”
“Tulipata nafasi ya kukutana ndani ya Square Circle na nilikuwa bora zaidi yake,” alisema.
Hivi karibuni aliitwa na rais wa UFC, Dana White, ambaye alipendekeza bondia huyo afanye pambano na Mrusi Khabib Nurmagomedov. Taarifa za pambano dhidi ya chipukizi nyota wa Kijapan linaweza kuwa ishara mpya kwamba Mayweather anafikiri kuhamia ndani ya MMA.
“Tulipata nafasi ya kukutana ndani ya Square Circle na nilikuwa bora zaidi yake,” alisema.
Hivi karibuni aliitwa na rais wa UFC, Dana White, ambaye alipendekeza bondia huyo afanye pambano na Mrusi Khabib Nurmagomedov. Taarifa za pambano dhidi ya chipukizi nyota wa Kijapan linaweza kuwa ishara mpya kwamba Mayweather anafikiri kuhamia ndani ya MMA.
Mayweather kuzipiga na Mjapan wa miaka 20
Reviewed by Zero Degree
on
11/06/2018 08:05:00 AM
Rating: