Mtolea achukua kadi ya CCM rasmi
Mtolea amechukua kadi hiyo leo Jumamosi, Novemba 24, katika Ofisi za CCM, Kidagaa Kata ya Buza jijini Dar es Saalaam na kukabidhiwa kadi hiyo na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Temeke, Almishi Hazali.
Mtolea ambaye alianza kwa kukabidhi kadi yake ya (CUF) kwa mwenyekiti huyo, amesema ameamua kujiunga na CCM ili aweze kushirikiana kikamilifu na Rais Dkt. John Magufuli katika katika ujenzi wa Taifa.
Novemba 15, 2018, Mtolea alijivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea alitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma.
Mtolea achukua kadi ya CCM rasmi
Reviewed by Zero Degree
on
11/24/2018 12:50:00 PM
Rating: