Malengo yetu ni kuwanyang’anya Simba ubingwa - Tambwe
Tambwe aliyewahi kuwa mfungaji bora kwenye misimu miwili ya ligi mabao yake mengine aliyafunga katika mchezo wa ligi na Singida United uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Spoti Xtra, Tambwe alisema; “Tunajua tunapitia kipindi kigumu hivi sasa wachezaji wa Yanga kwa maana ya hali ya kiuchumi tuliyokuwa nayo, lakini hali hiyo haitufanyi kukata tamaa na badala yake kuendelea kuipambania timu kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu.”
“Na malengo yetu ni kuwanyang’anya ubingwa Simba waliouchukua katika msimu uliopita, hivyo basi nilichopanga ni kuendelea kuitumia kila nafasi nitakayoipata kufunga mabao.
“Mabao niliyoyafunga mechi na Prisons yametokana na kujituma kwangu na kutambua umuhimu wa ushindi huo ambao utawaacha mbali wapinzani wetu katika malengo yetu tuliyojiwekea ya ubingwa msimu huu,” alisema Tambwe ambaye hivi karibuni alifunga ndoa hapa nchini.
Malengo yetu ni kuwanyang’anya Simba ubingwa - Tambwe
Reviewed by Zero Degree
on
12/07/2018 07:50:00 AM
Rating: