Waathirika VVU sasa kupelekewa ARV kwao
Imeelezwa kuwa lengo la mpango huo ni kuwarahisishia wagonjwa kuzifuata dawa hizo katika vituo vya afya.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyo fanyika kimkoa wilayani Mvomero, Mganga wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Frank Jacob, alisema hatua hiyo itawezesha wananchi wengi kujitokeza kupima afya zao kwa hiari na kutumia dawa hizo kwa wakati na kupunguza maambukizi mapya.
Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wagonjwa walioanzishiwa dawa hizo wakati mwingine kushindwa kufika katika vituo vya afya au hospitali kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kuogopa kunyanyapaliwa katika jamii.
Alisema kuwa ili kukabiliana na maambukizi mapya, mkoa umeamua kujipanga ili watakaopimwa na kubainika kuwa wameambukizwa VVU wataanza kupelekewa dawa hizo majumbani kwao.
Katika maadhimisho yaliyofanyika Manispaa ya Morogoro, mratibu wa kudhibiti Ukimwi wa Manispaa hiyo, Upendo Elias, alisema licha ya maambukizi hayo kuendelea kupungua bado kumekuwapo na changamoto ya kuongezeka kwa makundi maalum yenye tabia hatarishi.
Alisema takwimu zinaonyesha maambukizi ya VVU bado yapo juu kwa watu waliopima, huku kundi kubwa la wanawake likiongoza kulinganisha na la wanaume.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, aliwataka wanaume kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuacha tabia ya kujigamba na vipimo walivyopima wake zao kuwa wako salama.
“ Wapo wanaume wanatembea na vyeti vya majibu ya wake zao ambao wamepimwa na kuonekana wako safi, wanapaswa na wenyewe kwenda kupima wapate majibu yao, sio kutembea na majibu ya mke wake, hivyo natoa wito wanaume nao wakapime,” alisema.

Reviewed by Zero Degree
on
12/07/2018 08:13:00 AM
Rating: