Loading...

Mark Hughes awa meneja wa kwanza EPL kutimuliwa kazi mara mbili ndani ya mwaka mmoja


Meneja wa Mark Hughes amefutwa kazi baada ya kuhudumu kama meneja wa Southampton kwa miezi minane pekee.

Watakatifu hao wa St Mary's, waliotoka sare na Manchester United katika Ligi ya Kuu ya Uingereza Jumamosi, kwa sasa wanashikilia nafasi ya 18 kwenye jedwali.

Southampton wamethibitisha kufutwa kwake kupitia taarifa, na kuongeza kwamba : "Mchakato wa kumtafuta meneja mpya wa kuipeleka mbele klabu hiyo tayari umeanza."

Mkufunzi msaidizi wa kikosi cha kwnaza Kelvin Davis ataongoza timu hiyo kwa mechi yao dhidi ya Tottenham siku ya Jumatano.


Hughes, ambaye aliwahi kuchezea klabu hiyo ya pwani ya kusini mwa Uingereya, alijiunga na Southampton mwezi Machi, miezi miwili baada ya kufutwa kazi na Stoke City.

Southampton walikuwa alama moja juu ya eneo la kushushwa daraja wakati huo na mkufunzi huyo wa miaka 55 alikuwa aliwaongoza kujinusuru kwa kuwawezesha kushinda mechi mbili kati ya mechi zao nne za mwisho.

Hata hivyo, wametatizika msimu huu, na katika kipindi ambacho amekuwa nao, wameshinda mechi tatu pekee kati ya 22 walizocheza ligini.

Kabla ya kutoka sare na Manchester United, Southampton walicharazwa 3-2 na Fulham ambao pia wanakabiliwa na hatari ya kushushwa daraja. Aidha, waliondolewa Kombe la Ligi kwa mikwaju ya penalti na Leicester City.

Pamoja na Hughes, meneja msaidizi wa kikosi cha kwanza Mark Bowen na mkufunzi Eddie Niedzwiecki pia wameondoka katika klabu hiyo.
Mark Hughes awa meneja wa kwanza EPL kutimuliwa kazi mara mbili ndani ya mwaka mmoja Mark Hughes awa meneja wa kwanza EPL kutimuliwa kazi mara mbili ndani ya mwaka mmoja Reviewed by Zero Degree on 12/04/2018 12:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.